Home Lifestyle Entertainment Messi ajinunulia ndege maalum kwa usafiri wake

Messi ajinunulia ndege maalum kwa usafiri wake

1110
0
[ndege mpya ya mchezaji Lionel Messi.photo/kwa hisani]

Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya uhispania Barcelona, Lionel Messi,  agonga vichwa vya habari sio kwa umahiri wake uwanjani bali kwa kununua ndege mpya ya kifahari aina ya Gulfstream V ambayo itakuwa maalum kwa ajili ya usafiri wake na familia yake.

Ndege hiyo ya kibinafsi ambayo imemgharimu mshambuliaji huyo kitita cha takriban pauni milioni 15 sawia na takriban bilioni 1.5 za Kenya, ina idadi ya viti 16 ambavyo vinaweza kubadilishwa na kuwa vitanda nane.

Kutokana na umbo la ndege hiyo imeundwa kuwa na vyumba viwili vya bafu sawia na meko mbili za kupikia.

Miongoni mwa nakshi zinazoambatana na muundo wa kisasa wa ndege hiyo ni kuchorwa nambari 10, nambari ambayo Messi huvaa akiwa uwanjani.

Aidha ngazi za ndege hiyo zimeandikwa majina ya familia yake Messi, mke wake Antonela pamoja na majina ya watoto wake watatu ambao ni Thiago, Ciro na Mateo.