Home News Zingatieni maadili mnapo sherehekea krismasi-ashinikiza Kivuva

Zingatieni maadili mnapo sherehekea krismasi-ashinikiza Kivuva

434
0
Askofu mkuu wa kanisa katoliki jijini Mombasa Martin Kivuva amewashinikiza waumini wote wa dini ya kikristo nchini kusherehekea siku kuu ya kirismasi kwa kuzingatia maaadili ya kidini .
 
Kauli hii imetokana na kuwa wengi wa wafuasi wa dini hiyo wamekuwa wakikiuka mafundisho yanayoambatana na sherehe hiyo ya krismasi na badala yake kuingilia starehe na anasa zinazoenda kinyume na uhalisia wa siku hiyo.
 
Akizungumza na wanahabari baada ya dhwifa ya chakula cha mchana iliyoleta pamoja zaidi ya familia 400 za vijana wasio na makao mjini Mombasa, askofu Kivuva alisisitiza maadili mema miongoni mwa waumini wa dini ya kikristo hususan wakati huu wa sherehe za krismasi ikizingatiwa kuwa ni wakati mwafaka wa kuwahudumikia na kusaidia wasiojiweza katika jamii.
Huku akikemea maasi yanayotekelezwa na baadhi ya watu kwa madai ya kusherehekea siku hiyo, Kivuva ameonya utumizi wa mihadarati na ulevi kama vitu vinavyochangia pakubwa katika ajali na hata kuvunjika kwa familia.
 
Vile vile askofu huyo aliwahimiza waumini kuliombea  taifa la Kenya liendelee kuwa na amani na uwiano baina ya wananchi wa tabaka mbali mbali kama njia moja ya kufanikisha maafikiano ya rais Uhuru Kenyatta na kinara wa NASA Raila Odinga ili kuona kuwa maendeleo yanapatikana.
 
Kauli yake inajiri zikisalia siku mbili pekee waumini wa dini ya kikristo kuanza rasmi sherehe za krismasi.