Home Swahili Hub Mamlaka ya ubaharia nchini yateua Mkurugenzi mkuu mpya.

Mamlaka ya ubaharia nchini yateua Mkurugenzi mkuu mpya.

153
0
[Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya ubaharia nchini KMA George Nyamako(kushoto) wakati wa kuteuliwa kwake/picha-Mduney Husseiney]

Bodi ya Mamlaka ya ubaharia nchini (KMA) imemteua rasmi George Nyamoko Okong’o kama Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo.

Taarifa ya uteuzi huo imebainishwa na Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka hiyo Malika Ali akidokeza kuwa Mkurugenzi huyo mpya atachukua hatamu za uongozi wa Mamlaka hiyo katika kipindi cha Miaka 3 kama inavyoashiria kandarasi yake.

Akizungumza wakati wa hafla ya uteuzi, Mwenyekiti wa bodi hiyo alidhihirisha ukakamavu wa usimamizi wa bodi ya mamlaka hiyo ya ubaharia huku akisisitiza kuwa uteuzi huo ulitekelezwa kwa umakini sawia na kuangazia utaalamu wa hali ya juu.

“Mamlaka hii inamajukumu mazijo na tegemeo kuu katika ustawishaji wa rasilimali na uchumi wa baharini, ndiposa inahitaji usimamizi kakamavu katika uongozi wake,” alisema Malika.

Uteuzi wa George Nyamoka kama Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Ubaharia nchini ulikuja baada ya kuchukua nafasi ya George Mc’goye aliyekuwa kaimu mkurugenzi baada ya kuondoka kwa Nancy Karigithu ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu katika kitengo cha Maswala ya bahari na usafirishaji baharini.

Nyamoko alimiminiwa sifa ya kuweza kuimarisha utendakazi wa mamlaka hiyo kutokana na tajruba aliyo nayo ikizingatiwa kuwa amehudumu katika kikosi cha wanamaji nchini kwa takriban miaka 20 akistaafu katika kiwango cha meja.

Hata hivyo kwa upande wake Mkurugenzi mkuu huyo mpya, amehakiki ushirikiano mwema na wadau wote katika sekta hiyo ya ubaharia ili kuona kuwa malengo na ruaza waliyo nayo imefikiwa.

“Nimeshukuru kwa kupewa fursa hii kuhudumikia wananchi, najua safari inayotukabili ni ndefu isiyokosa changamoto ila natumai kwa ushirikiano wenu tutafanikiwa,” alisema Nyamoko.