Mahakama ya mjini Mombasa imemuhukumu mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi kifungo cha miaka minne gerezani baada ya kumpata na hatia ya kuwapiga na kuwajeruhi maafisa wawili wa polisi, Dennis Nambisia na Agapio Ndwiga wakati wa kura za mchujo za chama cha ODM mwezi Aprili mwaka uliopita .
Akitoa uamuzi huo hakimu wa makahama hiyo Evans Makori amesema kuwa upande wa mashtaka umetoa ushahidi wa kutosha kuonyesha wazi kuwa mbunge huyo alitekeleza kitendo hicho .
Makori aidha amefichua kuwa ushahidi huo pia umebaini kwamba mbunge huyo alishindwa kuwazuia wafuasi wake waliokuwa na ghadhabu dhidi ya kuzua vurugu na kuwapiga polisi hao .
Hakimu huyo amemuuagiza mwinyi kulipa faini ya shillingi millioni moja au atumikie kifungo hicho huku akiawaamurisha maafisa wa usalama kumzuilia mbunge huyo korokoroni hadi pale atakapo lipa faini hiyo .
Hata hivyo mahakama hiyo imemuondolea mwinyi mashtaka mengine saba yaliyokuwa yanamkabili ikiwemo kuhitilafiana na vifaa vya uchaguzi ,kuwazuia wasimamizi wa uchaguzi huo wa mchujo ,kutumia nguvu kupita kiasi miongoni mwa mashtaka mengine .