Home Swahili Hub Mfalme wa taarab Mzee Yusuf aahirisha tamasha lake

Mfalme wa taarab Mzee Yusuf aahirisha tamasha lake

1128
0
[Mfalme wa mirindimo ya taarab Afrika Mashariki. Mzee Yusuf. Picha /Kwa Hisani].

Mfalme wa Taarab nchini Tanzania na Kanda ya Afrika Mashariki Yusuf Mwinyi kwa jina maarufu Mzee Yusuf ameahirisha burudani la Taarab lililopaswa kufanyika siku ya Ijumaa Juma hili.

Mzee Yusuf ambaye aliasi muziki wa taarab mwaka wa 2018 lakini akashindwa kuvumilia na kutangaza rasmi kwamba anarudi ukumbini amesema kuahirishwa kwa burudani hilo zito kumetokana na kifo cha rais wa tatu wa Jamhuri ya Tanzania Benjamin William Mkapa.

Gwiji

Mzee Yusuf anayetambulika kwa vibao moto moto vya taarab Kama vile Nakshi Nakshi, Mpenzi chocolate miongoni mwa vingine vingi amesema hataweza kuwapatia mashabiki wake dozi kamili ya taarab waliyoikosa kwa kipindi cha miaka miwili sasa siku hiyo ya Ijumaa.

Amesewasihi mashabiki wake kuwa na subira kwani wataburidika usiku kucha tarehe 7 ya mwezi Agosti katika ukumbi wa Dar Live Mbagala katika mkesha wa nane nane.

Mzee Yusuf ambaye ameonekana katika picha mbalimbali akijiandaa kuwapatia tiba kamili ya muziki wa taarab mashabiki wake waliyo na hamu, amesema ni vyema kumpatia Mzee Mkapa aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 81 heshima anayostahili.

[Nguli wa muziki wa taarab Afrika Mashariki Mzee Yusuf. Picha/Kwa hisani].

Mzee Yusuf katika safari yake ya kurudi mjini atasindikizwa na wanamuziki tajika wa taarub akiwemo Malkia Leyla Rashid, Khadijah Yusuf, Fatma Mcharuko, Prince Amigo, Mtoto Pori miongoni mwa wengineo.

Ni tamasha ambalo linasubiriwa kwa hamu mno, huku wapenzi wa taarab kutoka Kanda ya Afrika Mashariki wakijiandaa kuhudhuria.