Home Swahili Hub Polisi wachunguza maafa ya watu wawili katika Bahari hindi

Polisi wachunguza maafa ya watu wawili katika Bahari hindi

970
0
[ Miili ya watu wawili iliyotolewa katika Bahari hindi katika ngome ya kitaifa ya Fort Jesus Mjini Mombasa. Picha/Maxwell Ngala]

Maafisa wa polisi Mjini Mombasa wameidhinisha uchunguzi kuhusu vifo vya watu wawili katika Bahari hindi.

Miili ya wawili hao imepatikana ikielea katika ufukwe wa Bahari eneo la makavazi ya kitaifa ya Fort Jesus siku ya Jumatano.

Kamanda mkuu wa polisi katika Kaunti ya Mombasa Johnston Ipara amesema kwamba haijabainika wazi iwapo watu hao walikuwa wakipiga mbizi ndipo wakalemewa na mawimbi na kusombwa na maji.

“Kulingana na Wale waliyokuwa ufukweni ni kwamba wanaume hao walikuwa watano japo watatu kati yao wakaponea na wawili wakapoteza maisha, japo tumeidhinisha uchunguzi,” akadokeza Ipara.

Hata hivyo tukio hilo limezua maswali hasa baada ya miili ya wawili hao kuwa na nguo zote na hata viatu kinyume na mavazi ya kawaida ya watu wanaojitosa majini kuogelea.

Miili ya wawili hao waliyo na asili ya kimaasai imepelekwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani huku uchunguzi ukiendelea.